Sunday, 7 August 2011

mwanza



taswira ya usiku kutoka ndani ya ndege

Dubai. Wakati unapiga picha ya aina hii usigusishe kamera kwenye kioo kwani mtikisiko utaharibu taswira

Taswira na watu mashuhuri

Ukikutana na watu mashuhuri usione noma kuomba kupiga picha nao, wengi wao hawana neno kwa hilo. Hapa Ankal akiwa na mwanamuziki Yvonne Chaka Chaka na mumewe mjini Sandton, Afrika ya Kusini

taswira za flashi na bila flashi

 Bila flashi
Na Flashi
Jaribu kupiga picha bila flashi na utaona matokeo yake kama inavyoonesha hapo juu. Tofauti ya upigaji ni kwamba ya bila flashi inabidi utumie stendi ama utulie sana wakati unafyatua na ya flashi unalenga na kupiga tu. Kwa wanaotumia automatic ama program saa zote hawana ujanja sana wa kuchunga uwezo wa kamera na flashi hata ikiwa kubwa. Hivyo sio vibaya kucheza na flashi kwa kutumia manual settings, ama bila flashi kwa manual settings

taswira za kampeni za uchaguzi mkuu 2011




kutoka katika jicho la ndege

usawa wa kijinsia katika kazi

Taswira toka sillicon valley, kitovu cha teknolojia, Palo Alto, California

 Ankal akiwa makao makuu ya Google Sillicon valley. Yafuatayo ni baadhi ya majengo ya makao makuu ya magwiji  teknolojia




kumbukumbu ya kocha wa Taifa Stars toka Brazil Marcio Maximo

 Maximo na wachezaji wake. Kuja kwake nchini kulileta msisimko wa aina yake katika soka, hadi alipoondoka
 Wachezaji na viongozi mazoezini. aliyesimama kushoto ni Meneja wa Taifa Stars Leopard Tasso Mukebezi na kocha msaidi Ally Bushiri

Mzee Hozza na mapacha wake kazini

Muasisi wa vikumndi vya matrumbeta kwanye maharusi Mzee Hozza akiwa na wanawe mapacha kazini

askari polisi kikosi cha kuzuia fujo kazini mjini Morogoro

 Ubabe...
Upole

taswira ya kumbukumbu ya kihistoria tanzania

Ni vyema kuhifadhi vyema kumbukumbu za aina hii kwa faida ya vizazi vya leo na baadaye. Nawasifu sana wapiga picha na wasafisha picha wa enzi hiyo kwa uhodari wao sio tu wa kupata taswira nzuri kama hizi bali pia kwa kuzihifadhi vyema kiasi ya kwamba hata rangi zake hazijachuja.

Saturday, 6 August 2011

Taswira toka kwa Balozi Peter Kallaghe

 Tunafurahi na kushukuru sana sana kwamba mdau wa kwanza aliyetuletea taswira zake sasa hivi baada ya TASWIRA ZETU kuibuka upya ni Balozi wetu Uingereza, Mh. Peter Kallaghe, ambaye wakati akiwa mapumzikoni Bagamoyo alikamata taswira hizi ambazo ameona ashee nasi. Shukran sana Mh. Balozi kwa kutufungulia pazia, nasi tunatumai kwamba wadau wa taswira watafuata nyayo ili tujinome kama hivi...

Supa modo Millen Magesse akiwa kazini










Hii ilikuwa ni katika Africa Fashion Week mjini Sandton Afrika ya Kusini ambako pamoja na kuwapoga picha Millen na Flaviana pia Ankal alipata kismati cha kula nao Konozzzz..

kutumia mwanga halisi kuna raha yake

Quality Centre shopping mall, Dar es salaam

sio lazima wapigwa picha wawe katikati ya taswira

Faida ya telephoto lens na mwanga halisia pamoja na taimingi

Nini uzuri ama ubaya wa taswira hii ya The Kilimanjaro Band 'Wana Njenje'

Jibu: Mpiga pich hakuwa makini. Kuna watu wawili wameharibu pozi kwa kuangalia kusiko...Fundisho hapa ni kwamba mpiga picha lazima afanye juu chini macho ya wote yaelekee kumoja...

Jicho la pili...

siku mwili wa mwalimu uliporejeshwa toka Uingereza

Ankal aliipata taswira hii kutoka daraja la Manzese jijini Dar es salaam. alipatya kazi kubwa kufikiria na mapema engo gani  nzuri itayoeleza siku hii kwa kuchanganya mambo yote muhimu ikiwa ni pamoja na umati wa watu, barabara, usafiri uliotumika pamoja na jeneza. Baada ya kupigwa na jua kwa masaa kama manne hivi Ankal alizawadiwa na taswira hii. Fundisho hapa ni kuwaza na mapema aina ya picha inayofaa kabla.

vikombe dukani

Raha kama hii ya bwana harusi akielekea kuoa usiache ikupite hivi hivi tu

usafiri Dar es salaam

Asante Da'Chemi Chemponda kwa taswira hii ambayo inapeleka watu wengi mbali sana bali pia kwa kizazi kipya cha daladala kinaona nini maada ya UDA inayotawala vyombo vya habari kwa sasa. Mdau tuteletee taswira za kumbukumbu kama hizi nasi tufaidi

Taswira za enzi hizo

Taswira ya kukumbukwa

Ankal na wenzie walipata bahati kulala siku moja katika jumba la Big Brother Africa mwaka jana. Tuletee taswira za kumbukumbu namna hii

Close up husaidia kuelezea hisia za mhusika