Oliver Mutukudzi akitumbuiza Dar es salaam
TASWIRA ZETU
Huu ni uwanja wa taswira. Mdau ambaye ni mpenzi wa picha unakaribishwa kuchangia picha, maoni, maswali, darasa, ukosoaji wa kujenga na kila jambo linalohusu fani hii. Endapo una lolote la kutuma lete kupitia issamichuzi@gmail.com nawe utahudumiwa. Tafadhali lete picha uliyopiga mwenyewe...
Wednesday, 17 August 2011
Tuesday, 16 August 2011
JK na Mbowe
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akipongezwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe baada ya kupishwa kuwa Rais wa awamu ya nne, huku Mzee Reginald Mengi askisubiri zamu yake
mechi ya Simba SC na Cosmopolitan
Kipa wa Simba Semainda akidaka mpira mbele ya mshambuliaji hatari wa Cosmopolitan Jumanne Masimenti huku mlinzi wake Omari Choggo Mluya "Choggo Chemba" akimlinda uwanja wa Ilala (siku hizi Karume)
Thursday, 11 August 2011
Ankal akiwa loliondo wakti wa sakata la Loliondo gate
Hapa ni Loliondo Guest House alimofikia Ankal wakati wa kufuatilia sakata la Loliondo gate miaka ya 90
Simba wa vita uwanjani
Hayati Mzee Rashidi Mfaume Kawawa akichezesha mechi ya wabunge na mawaziri uwanja wa Ilala (siku hizi Kumbukumbu ya Amani Abeid Karume)
ukarabati wa kwanza wa uwanja wa Uhuru
Uwanja huu hivi sasa unakarbatiwa kwa mara ya pili kujiandaa na sherehe za miaka 50 ya Uhuru. Katika ukarabati huu wa sasa jukwa la Green Stendi kushoto limevunjwa lote na linajkengwa upya sambamba na majukwa mengine uoande wa Urusi na kusini na kaskazini
Mwalimu akiwa na mwagwiji wa taswira wa enzi hizo
Toka shoto ni Max Madebe (Mfanyakazi), Sam Mmbando (Shihata), Vicent Urio (Daily News), John Makwaia (Maelezo), Mwalimu, Mwanakombo Jumaa (Maelezo), Wataalamu wa TFC, Adinani Mihanji (Shihata), John Lukuwi (Maelezo). Chini toka kulia ni Raphael Hokororo (Maelezo) Moshi Kiyungi (Maelezo), Boaz Mpazi (Maelezo), Charles Kagonji (Maelezo) na mdau
taswira toka mtwara na Mikindani
Asalaam alaykhum ankal,
Pokea taswira hizi za mji wa mtwara na mji mdogo mkongwe wa Mikindani.
From Chef Issa
chuma hiki alilala dr livingstone
chumba hiki alilala chief mkwawa
eneo hili lilitegwa kwa mazishi ya marehemu wa asili ya kihindi toka miaka ya 1820
Hapa ni maeneo maarufu ya feri kunapouzwa samaki na pia kuna kivuko cha kwenda kisiwa cha Msanga mkuu, Mtwara
hapa ni mbele ya jengo la old boma mikindani
Hapo aliposimamam huyo kijana apalikua na shimo lililotumika kutupia miili ya waliokwisha kunyongwa na inateleza mpaka baharini.
Nyumba ya Sharifu ambapo Mwalimu Nyerere alifikia na kuombea dua |
Chumba cha Dr Livingstone
hapa ndipo ilipokua eglish medium school na waliposoma watoto wa wakubwa tu na kwa sasa inatumika kama madrasa ya watoto wa kiislamu
mabaki ya mizinga iliyokua ikitumia wakati huo wa mjerumani kwa kujiham
Hii ndio nyumba aliyolala Mwalimu Nyerere alipokwenda mikindani enzi hizo pia aliombwe dua hapa na sharifu aliekua akiishi humo
hii ndio old boma
Mtwara Airport
Hii ni historia fupi ya utambulisho wa jengo la old boma
Hili jengo lilitumika miaka ya 1820 mpaka sasa kuchomea miili ya marehemu wa dhehebu ya baniani
Jumba la sinema Mikindani leo
Ndani ya Old Boma, mikindani
Msikiti wa dhehebu la shia uliojengwa toka mwaka 1901 mjini Mikindani
Old Boma
mfereji uliokua unatumika kupitishiwa watumwa chini kwa chini mpaka baharini ilipopaki jahazi
Huu ni mtaa maaarufu wa madukani ya wahindi na ofisi nyingi kubwa Mtwara
Ufukweni Mikindani
Jengo hili alilala Dr Livingtone kabla ya safari yake ya mwisho kuelekea zambia mauti yalipomkuta ambapo hivi sasa linakarabatiwa
jengo hili lina historia kubwa sana maana limejengwa pande nne na limejengwa na wakoloni wa kijerumani, kiingereza, kiarabu na Waafrika |
Jiwe hili lilitumika kama kipimo kwa watumwa ukiweza kuinua ulikua unauzwa kwa bei poa kabisa
Jumba hili lilikua soko la watumwa
Katika jengo la old boma hiki ndio chumba alicholalal mwalimu nyerere
Kule juu kabisa ndio maeneo ya old boma alipokua akikaa Dc wa kijerumani
kulia ni mahakama na kushoto ni mti uliotumika kunyongea watuhumiwa
kwenye lango la kuingia old boma utakuata mizinga miwili ya nyuki ikisema nyuki wadogo wasiouma
Watalii kibao
Msikiti wa dhehebu la shia uliojengwa toka mwaka 1901 mjini mikindan
mandhari ya jiji la mtwara kwa juu
Nyumba aliyoishi Dr David Livingtsone
na hapa ndio chuo kikuu cha SAUT Mtwara
Chumba alicholala Gavana
Old boma ilijengwa na wajerumani mwaka 1895
Inajieleza
sehemu hiii ndio ilikua ya anakaa mpokea pesa baada ya kuuza watuma |
Mandhari toka Old Boma Mikindani
Subscribe to:
Posts (Atom)