Tuesday 9 August 2011

Taswira za utalii wa ndani toka kwa Lijocha Nalitolela

Katika kuendeleza utalii wa ndani, nilipata nafasi ya kutembelea mbuga ya Ruaha mkoani Iringa. Tafadhali wawekee wadau nao wapate nafasi ya kuona picha za hazina tulizonazo katika nchi hii...pale ambapo picha zinaonekana kufifia, naomba nisamehewe, picha hizi zilichukuliwa na kamera ya simu ya N97, kwa hiyo sikuwa na control sana ya mazingira zaidi ya kutegemea jua tu.
Mdau Lijocha Nalitolela
Female Kudu
Familia ya viboko
Mamba wakiogelea
Watoto wa simba wakimngojea mama arejee toka "shopping" ya msosi
Ndege aina ya Shole
Zebras wakitoka kunywa maji
Velvet Monkeys
 Swala (Gazelles)
Twiga
Tembo
Mzee wa nyika mwenyewe, Simba...mwingine yupo kwa nyuma ya mti haonekani vizuri
======================================================
Mdau Lijoche!
Asante sana kwa yaswira hizi mwanana, ukichukulia umizidaka kwa simu ya mkononi. Hii inatia moyo sana kwamba kumbe kuna wadau ambao wako gado kuendeleza Libeneke la TASWIRA ZETU. Hongera sana na wala usisite siku ingine kutuletea taswira kama hizi kwani ni nzuri na hazina matatizo katika kuonesha utajiri wa maliasili ya nchi yetu. Endeleza Libeneke mdau, na wala usijali kuhusu aina ya kamera unayotumia. Kungekuwa na wadau 10 tu wa aina yako mambo yangekuwa mswano sana. Wewe ni mfano wa kuigwa.
-Michuzi

No comments: