Sunday 7 August 2011

taswira kutoka kwenye fiesta 2011

Ahmad Michuzi kaleta taswira hizi leo akiwa anasema kazipiga kwenye matamasha ya Fiesta kutaka kuonyesha ni namna gani unaweza kutumia mwanga halisi kuinasa taswira yako badala ya Mwanga wa Flash,ingawaje wafungaji taa wengi kwenye matamasha hawazingatii umuhimu wa Mwanga kwa mpiga picha,Wao wanachojua ni kumulika eneo husika basi, hawana elimu ya light set up ya kutosha kwa kuzingatia mambo mengi kwa upana.Hivyo kama mpiga picha wewe na camera yako elewa mazingira yako ya kazi na tumia kifaa chako ipasavyo.



 


Ankal anasema: Hongera kwa taswira nzuri. Ila kama ujuavyo unapokamata kamera na kuingia nayo mitaani ni sawa na dereva kuwasha gari na kuingia barabarani ambako fanya ufanyalo trafiki akikusimamisha hakosi kosa hata kama gari ni jipya. Hivyo kaa chonjo nikuchambulie taswira moja baada ya ingine.

1. Taswira ya kwanza nzuri lakini hujaitendea haki kadamnasi. Achana na program ama automatic settings. Jaribu manual na cheza na f.stops. Yaani ungeseti katika manual, halafu cheza na ISO settinngs (hapo 400 ASA ama 800ASA ingefaa), na spidi ungeshusha hadi f8 ama f4 hivi) ungefanikisha.

2. Taswira ya pili nzuri ila mtaa wa juu kulia umetibua. Hapo sina uhakika ulitaka kuonesha hiyo taa ama sura ya msanii. Chagua kimoja (Sura ama Taa) unachotaka kusisitiza ndio kiwe chenye umbele katika muonekano.

3. Taswira ya binadamu bila uso wa mwenyewe kuonekana, japo kiduchu tu,  huwa inakuwa maiti.

4. Rejea namba 3

1 comment:

Anonymous said...

Bwana michuthi napingana na wewe unapozungunmzia settings hapo juu;
1) Spidi sio F pointi - spidi au shutter speed ni kama neno lenyewe ni muda unaoruhusu mwanga kuingia katika kamera yako. Hii sana hutumika katika film photography.
Wataalamu hutumia spidi kutoa taswira ambazo husimamisha kitendo au kukiendeleza (blur effect) ambacho hakionekani kwa macho ya binadamu.

2)F pointi ni tundu katika lens ambalo huruhusu mwanga kuingia katika kamera. Mchanganyiko wa spidi na hili tundu huto taswira.

3)Ndugu Ahmed yupo kwenye mwanga halisi. F pointi yake inatakiwa iwe ndogo kabisa( Hii inategema na uwezo wa lens yake). Wataalamu wa picha hizi hutumia sana lens aina F2.8 200mm. Wanahakikisha kwamba wanafungua jicho (F pointi) kutokana na uwezo wa lens ili kutumia spidi ndogo ambayo huwezesha angalau kutotikisa taswira.

3) Nakubaliana na wewe na ISO settings, lakini naona kama unaiogopa. Sina uhakika ndugu Ahmed anatumia kamera gani lakini kwa DSLR nyngi unaweza cheza na ISO mpaka 3200 bila ya taswira kuwa na mchele.

4)Kwa ufupi mpiga picha hizi anaonekana ni kama anaibia. kama msanii anayesubiri zamu yake ku perform. Kama kaka Michuzi unavyosema bila sura picha ni maiti.