Thursday 11 August 2011

taswira toka mtwara na Mikindani

Asalaam alaykhum ankal,
Pokea taswira hizi za mji wa mtwara na mji mdogo mkongwe wa Mikindani.
From Chef Issa

 chuma hiki alilala dr livingstone
 chumba hiki alilala chief mkwawa
 eneo hili lilitegwa kwa mazishi ya marehemu wa asili ya kihindi toka miaka ya 1820
 Hapa ni maeneo maarufu ya feri kunapouzwa samaki na pia kuna kivuko cha kwenda kisiwa cha Msanga mkuu, Mtwara
 hapa ni mbele ya jengo la old boma mikindani
 Hapo aliposimamam huyo kijana apalikua na shimo lililotumika kutupia miili ya waliokwisha kunyongwa na inateleza mpaka baharini.



Nyumba ya Sharifu ambapo Mwalimu Nyerere alifikia na kuombea dua
 Chumba cha Dr Livingstone
hapa ndipo ilipokua eglish medium  school na waliposoma watoto wa wakubwa tu na kwa sasa inatumika kama madrasa ya watoto wa kiislamu
 mabaki ya mizinga iliyokua ikitumia wakati huo wa mjerumani kwa kujiham

 Hii ndio nyumba aliyolala Mwalimu Nyerere alipokwenda mikindani enzi hizo pia aliombwe dua hapa  na sharifu aliekua akiishi humo
 hii ndio old boma
 Mtwara Airport
 Hii ni historia fupi ya utambulisho wa jengo la old boma
 Hili jengo lilitumika miaka ya 1820 mpaka sasa kuchomea miili ya marehemu wa dhehebu ya baniani
 Jumba la sinema Mikindani leo
 Ndani ya Old Boma, mikindani
Msikiti wa dhehebu la shia uliojengwa toka mwaka 1901 mjini Mikindani
 Old Boma
  mfereji uliokua unatumika kupitishiwa watumwa chini kwa chini mpaka baharini ilipopaki jahazi
 Huu ni mtaa maaarufu wa madukani ya wahindi na ofisi nyingi kubwa Mtwara
 Ufukweni Mikindani
Jengo hili alilala Dr Livingtone kabla ya safari yake ya mwisho kuelekea zambia mauti yalipomkuta ambapo hivi sasa linakarabatiwa


jengo hili lina historia kubwa sana maana limejengwa pande nne na limejengwa na wakoloni wa kijerumani, kiingereza, kiarabu na jengo hili lina historia kubwa sana maana limejengwa pande nne na limejengwa na wakoloni wa kijerumani, kiingereza, kiarabu na Waafrika

 Jiwe hili lilitumika kama kipimo kwa watumwa ukiweza kuinua ulikua unauzwa kwa bei poa kabisa
 Jumba hili lilikua soko la watumwa
 Katika jengo la old boma hiki ndio chumba alicholalal mwalimu nyerere
 Kule juu kabisa ndio maeneo ya old boma alipokua akikaa Dc wa kijerumani
 kulia ni mahakama na kushoto ni mti uliotumika kunyongea watuhumiwa
 kwenye lango la kuingia old boma utakuata mizinga miwili ya nyuki ikisema nyuki wadogo wasiouma
 Watalii kibao
 Msikiti wa dhehebu la shia uliojengwa toka mwaka 1901 mjini mikindan
 mandhari ya jiji la mtwara kwa juu
 Nyumba aliyoishi Dr David Livingtsone
 na hapa ndio chuo kikuu cha SAUT Mtwara
 Chumba alicholala Gavana
 Old boma ilijengwa na wajerumani mwaka 1895
 Inajieleza
sehemu hiii ndio ilikua ya anakaa mpokea pesa baada ya kuuza watuma
Mandhari toka Old Boma Mikindani

2 comments:

Anonymous said...

Serikali imeyatupa maeneo haya ingeyajali kuna vivutio vingi na kuna mandhar nzuri pia ingepunguza msongamano dar lakini wapi ndio mwafrica nyumba za maana ni zile walizojenga wazungu na waarabu inasikitisha mji wa zamani namna hii kuwa hivi.

Nyamonde R said...

Katika tasnia ya ujenzi ni vyema kuhakikisha kuwa kila jengo lenye historia linatunzwa kwa kuwashirikisha wataalam wenye taaluma hiyo na hao wapo tatizo ni kuwa wale wenye madaraka hawaoni umuhimu wa kufanaya hivyo ndio maana hata bajeti ya jambo hilo huwa ni finyu sana, na kama tutakuwa na umakini kwenye hilo suala basi wanafunzi wetu watapata kujua vitu vingi na kujifunza pia.