Monday 6 October 2008

kamera gani bomba kununua?

Mara kwa mara nimekuwa napata maswali ya je, ni kamera gani bomba kununua. Jibu huwa nashindwa kutoa mara moja, kwani kila mtu ana nia tofauti katika matumizi ya kamera. Hebu tuangalie baadhi ya mwaswala muhimu ya kuangalia unapotaka kujitosa dukani.

Kununua kamera ya dijito ama vifaa vyovyote vya upigaji picha kunachanganya akili kiasi. Na kama ndio unanunua kamera kwa mara ya kwanza, unaweza ukaparaganyikiwa kwani zipo aina kibao. Hata hivyo, usikonde, kabla ya kuangalia bei ama aina ya kamera, hebu fikiria kwanza unataka kuitumia namna gani hiyo kamera?

1. Je utakuwa unapiga picha za ndani zaidi kuliko nje. Basi jibu hapo litakupeleka kwenye kujua aina gani ya flashi unayohitaji.
2. Je utakuwa unapiga taswaira zilizoganda kama vile samani za ndani ama unataka kupiga picha za haraka kama vile za michezo? Hapo utapata akili ya aina gani ya lenzi inakufaa
3. Je utakuwa unapiga picha zenye kuonesha sehemu pana kama vile milima na mabonde iliyo mbali ama picha za ndani kama vile za watu maua ama wanyama. Hapa utajua kama utahitaji lenzi yenye zuum ama yenye engo pana (wide angle) ama ya vitu vya karibu.
4. Je, unatak kamera kama mtumiaji wa kawaida tu wa picha za nyumbani za binafsi, ama za biashara. Hapa utatakiwa kujua kwamba unahitaji kamera yenye vikorokoro vya aina gani.
5. Je, ukishapiga hizo picha utakuwa unazikuza ama kuzihifadhi kwenye nyaraka katika kompyuta yako, ama utachapa kwenye tovuti, ama kutuma kwa email, ama kufanyia presentation? Hii itakupa akili ya kamera ya ukubwa gani kwa maana ya pixel (picture elements) zinazohitajika.

Njia ingine bora ya kufikiria kabla ya kununua kamera ni je, unataka ya kubeba mfukoni ama kuning'niza shingoni ama kubeba mkononi? Hili nalo ni muhimu ukizingatia shughuli unazofanya. Kama wewe ni mtu bize na mambo mengine nje ya picha ya mfukoni itakufaa.
kama ndiyo kazi yako kupiga picha basi ya kubeba shingoni ama begani ama mkononi ni saizi yako.
Lakini muhimu kuliko yote hayo ni mfuko wako. Yaani je una shi'ngapi tayari kununulia kamera? Usijetaka benzi wakati uwezo wako ni kombi. Nadhani nasomeka hapo.
Kwa msaada wa haraka haraka hebu pitia orodha hii chini ya tovuti za makampuni yanayotengeneza kamera ujaribu kuona nini kitakufaa:

1 comment:

Anonymous said...

Michuzi,
mimi Ninapendelea kupiga picha ambazo zina fall ktk category 3 of the 'Michuzi Classification'.

Ni Kamera gani zinafaa picha za category hii. Ubebaji (Portability) sio shida kwangu. Quality ndio

For a long time nimekuwa nikitumia Kodak Z512 & Z612.

Mdau,
5524253